1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Palestina yapinga kuwepo kwa al-Qaeda katika ukanda wa Gaza

20 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQ1

Mamlaka ya Palestina imekanusha madai yaliyotolewa na makachero wa Israel kwamba wanamgambo kutoka mataifa ya kigeni walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, waliingia ukanda wa Gaza baada ya Israel kuondoka mwezi uliopita.

Kiongozi wa ukachero nchini Israel alitangaza juma hili kwamba wapiganaji wa jihad waliingia Gaza wakati wa machafuko katika mpaka na Misri kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka eneo hilo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Palestina amesema kufuatia uchunguzi uliofanywa na maofisa wa usalama wa Palestina hakuna wanachama wowote wa kundi la al-Qaeda wanaoishi katika ukanda wa Gaza.