1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY:Kundi la hamas laionya serikali dhidi ya kuwapokonya silaha

1 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfJ

Kundi la Hamas leo limeionya serikali ya Palestina dhidi ya kuwapokonya silaha wanamgambo wake.

Kundi hilo limesema kwamba serikali wala isithubutu kamwe kuwapokonya silaha kwa nguvu la sivyo itawatambua wao ni kina nani na wana uwezo wa kiasi gani.

Lakini hata hivyo Ahmed AL- Jaabari kiongozi mmoja wa viongozi wa kundi hilo amekanusha madai kwamba kundi hilo linatafuta mzozo na serikali ya Palestina.

Kundi jingine la Al-Aqsa Martyrs pia limearifu halitoweka chini silaha zake hata baada ya Israel kukamilisha mpango wake wa kuondoka Ukanda wa Gaza.

Rais wa Palestina yupo chini ya shinikizo kutoka Israel za kumtaka ayavunje makundi ya wanamgambo nchini Palestina.