1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Burundi yamkamata Gavana wa Benki Kuu kwa kuhatarisha uchumi

11 Oktoba 2023

Gavana wa benki kuu nchini Burundi Murengerantwari Dieudonné ametiwa nguvuni akituhumiwa kuhatarisha uchumi wa nchi.

https://p.dw.com/p/4XOVI
Rais wa Burundi  Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye Picha: Bujumbura Amida Issa/DW

Hakimu mkuu wa Burundi Manirakiza Leonard amesema mkuu huyo wa benki kuu pamoja na mfanyabiashara  Niyonsaba Sylvestre wanatuhumiwa kuhatarisha uchumi wa taifa, wizi na rushwa.

Uchunguzi kuhusiana na madai hayo bado unaendelea. Ni mwaka mmoja  tangu gavana huyo mwenye umri wa miaka 38 kukabidhiwauongozi wa benki kuu ya nchi hiyo.

Soma pia:Uchumi wa dunia wayumba - IMF

Tayari Rais Evariste Ndayishimiye amemteuwa Bigendako Edourd Norma kuongoza benki hiyo.

Hayo ni wakati IMF imetangaza kuwa uchumi wa Burundi uko pabaya sanaa na kwamba fedha za kigeni ni sawa na asilimia 0,5 na nchi hiyo haina bidha inaozouza nje ya nchi.