1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Gabon yapigia kura katiba mpya baada ya mapinduzi

16 Novemba 2024

Gabon inapiga kura ya maoni kupitisha katiba mpya, zaidi ya mwaka mmoja baada ya askari waasi kumpindua rais wa muda mrefu wa nchi na kunyakua madaraka katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Afrika ya Kati.

https://p.dw.com/p/4n4nm
Gabon | Jenerali Brice Oligui Nguema
Gabon inapiga kura ya maoni kupitisha katiba mpya.Picha: AFP/Getty Images

Takriban watu milioni 1 wanatarajiwa kupigia kura rasimu ya katiba, ambayo inapendekeza mabadiliko makubwa ambayo yanaweza kuzuia utawala wa nasaba na uhamisho wa madaraka, na inahitaji zaidi ya 50% ya kura ili kupitishwa.

Soma pia:Viongozi wa kijeshi wa Gabon watangaza kuandaa uchaguzi 2025

Rasimu hiyo ya katiba inaweka muhula wa miaka saba, unaoweza kurefushwa tu mara moja, badala ya katiba ya sasa inayoruhusu mhula wa miaka mitano bila ya kikomo. Pia inasema wanafamilia hawawezi kurithi urais na kuwania nafasi ya waziri mkuu.

Soma pia: Kiongozi wa kijeshi Gabon ateuwa wabunge wapya wa Bunge la Kitaifa

Mnamo 2023, wanajeshi wa Gabon walimpindua Rais wa muda mrefu Ali Bongo Ondimba na kumtangaza mkuu wa jeshi, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema, kama rais wa kamati ya mpito kuongoza nchi.