1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa kijeshi wa Gabon watangaza kuandaa uchaguzi 2025

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2023

Viongozi wa kijeshi wa Gabon waliomwondoa madarakani Rais Ali Bongo Ondimba, wametangaza kuwa wanakusudia kufanya uchaguzi mnamo mwezi Agosti mwaka 2025.

https://p.dw.com/p/4Ym36
Gabon, Libreville | Kiogozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali  Brice Oligui Nguema.
Kiogozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema.Picha: AFP/Getty Images

Msemaji wa serikali Ulrich Manfoumbi alitangaza mipango ya kufanyika uchaguzi na kumaliza kipindi cha mpito wakati wa hotuba yake ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya taifa.

Amesema baraza la mawaziri limepitisha muda wa mpito ambao utahitaji kuidhinishwa katika kongamano la kitaifa, litakalofanyika Aprili mwaka ujao na kujumuisha wadau wote muhimu kote nchini.

Soma pia: Jenerali Nguema aapishwa kuwa rais wa Gabon

Kiongozi wa mapinduzi Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye aliapishwa kama rais wa mpito, ameahidi kurejesha nchi katika utawala wa kiraia. Nguema aliongoza mapinduzi dhidi ya Ali Bongo mnamo Agosti 30.

Mapinduzi hayo yalifanyika muda mfupi baada ya Bongo ambaye familia yake imetawala Gabon kwa miaka 35, kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais ambao jeshi na upinzani, walitangaza kuwa uligubikwa na udanganyifu.