1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon yakubali mwongozo wa kurejea kwenye demokrasia

7 Septemba 2023

Mpatanishi wa kanda ya Afrika ya Kati na utawala mpya wa kijeshi wa nchi hiyo Jenerali Brice Oligui Nguema wamekubali kuandaa mwongozo wa kurejesha utawala wa kidemokrasia baada ya mapinduzi ya wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4W4sO
Jenerali Brice Oligui Nguema
Jenerali Brice Oligui NguemaPicha: AFP/Getty Images

Jenerali Nguema aliapishwa siku ya Jumatatu kama rais wa mpito baada ya kuongoza mapinduzi ya Agosti 30 ambayo yalimaliza utawala wa nusu karne wa familia ya Bongo.

Soma zaidi: Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon asema hatakimbilia kuitisha uchaguzi

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) ilimtuma mjumbe wake, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera, mjini Libreville kwa mazungumzo na Oligui.

Hata hivyo hakukuwa na maelezo zaidi kuhusu lini mchakato huo utaanza. Jenerali Nguema siku ya Jumatatu aliahidi kuandaa "uchaguzi huru, wazi na wa kuaminika" ili kurejesha utawala wa kiraia lakini hakutoa muda uliopangwa.