FIFA and UEFA yaifungia Urusi kushiriki michezo
1 Machi 2022Haya yanajiri baada ya Shirikisho la soka duniani FIFAna Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kusimamisha vilabu na timu za kitaifa za Urusi kutoka kwa mashindano yote hadi watakapopewa taarifa zaidi.
Uamuzi wa kuizuia Urusi kushiriki katika michezo inajiri baada ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa kuyataka mashirika ya michezo kuwatenga wanariadha wa Urusi na maafisa kutoka hafla za kimataifa, pamoja na Kombe la Dunia la soka kwa kile walichotaja kama kulinda uadilifu wa mashindano ya michezo ya kimataifa na usalama wa washiriki wote.
soma FIFA yaipiga marufuku Kenya katika soka ya kimataifa
Uamuzi huo ulifungua njia kwa FIFA, bodi inayoongoza kandanda, kuiondoa Urusi kwenye Kombe la Dunia kabla ya mechi ya mchujo iliyoratibiwa Machi 24 ambayo Poland tayari imekataa kucheza dhidi ya Urusi.
Urusi yapokonywa uenyeji
Aidha Urusi imekatazwa kushiriki au kuwa mwenyeji wa michezo yoyote duniani. Hata hivyo haikuwa wazi jinsi gani uamuzi huu utaathiri wachezaji wa mpira wa magongo wa Urusi katika Ligi ya kitaifa ya mchezo wa magongo (NHL) na wachezaji wa tenisi, ikiwa ni pamoja na Daniil wa Medvedev, katika mashindano ya Grand Slam, ATP na WTA ambayo yapo nje ya mamlaka ya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi.
Kamati kuu ya Raga Duniani iliipiga marufuku Urusi na Belarus kutoka kwenye shughuli zote za kimataifa za raga ikisema inalaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na Belarus kwa kuisaidia katika hatua hii.
soma UEFA kuivua Moscow uenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa
Shirikisho la Soka la Urusi (RFU) katika taarifa yake limesema hatua hizo ni kinyume na viwango na kanuni zote za mashindano ya kimataifa dhidi ya maadili ya ari ya michezo na haki ya kucheza.
Hatua ya FIFA na UEFA pia ni ufanisi kwa timu ya soka ya Ujerumani RB Leipzig kwani imewapata nafasi ya kutocheza dhidi ya Spartak Moscow kwenye michuano ya robo fainali ya Ligi ya Ulaya na kuzuia Urusi kushiriki Kombe la Dunia mechi za mchujo baadaye mwezi huu.
Shirikisho la Soka la Urusi limedai uamuzi huo ulikuwa wa kibaguzi na kusema inaweza kukata rufaa chini ya sheria ya kimataifa ya michezo, katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo.
Timu ya Ujerumani Schalke 04 wiki iliyopita ilitangaza kuondoa nembo ya kampuni ya Urusi ya Gazprom kutoka kwenye sare zao na jana jumatatu klabu hiyo ilitangaza kwamba usimamizi wake umeamua kusitisha mkataba wake na kampuni hiyo ya Urusi ambao imekuwa na ushirikiano nao kwa miaka 15.