1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FDD wanapinga raia kupokonywa silaha kwa nguvu

11 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEh

Waasi wa zamani wa kutoka chama cha FDD wamepinga uamuzi wa rais Ndayizeye wa Burundi wa kuwapokonya silaha kwa nguvu raia.Wanahoji uamuzi huo unaweza kuzusha hali ya mtafaruku .Mkuu wa FDD Pierre Nkurunziza amewaambia waandishi habari wanapendelea utaratibu wa kuwapokonya raia silaha uambatane na makubaliano jumla ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2003.Wanataka pia mpango huo usimamiwe kama ilivyopangwa na tume ya Umoja wa mataifa nchini Burundi Onub.FDD inataka kwanza chaguzi ziitishwe kabla ya wananchi kupokonywa silaha. Chaguzi tano zinatazamiwa kuitishwa nchini Burundi hadi Agosti 19 ijayo,ikiwa ni pamoja na chaguzi za bunge na rais.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoripuka mwaka 1993 vimeshagharimu maisha ya zaidi ya watu laki tatu,wengi kati yao ni raia wa kawaida.