1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

FAO: Idadi ya wahanga wa njaa imeongezeka

24 Januari 2023

Shirika la kilimo na chakula duniani - FAO pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yamesema idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa upatikanaji wa chakula barani Asia inaongezeka.

https://p.dw.com/p/4Mckc
Kenia Marsabit Pastoralismus
Picha: DW/Michael Kwena

Ripoti ya mashirika hayo imesema bei za vyakula pia zinazidi kupanda hali inayosababisha kiwango cha umasikini kuongezeka miongoni mwa watu wa bara hilo.

Ripotihiyo imelitaja janga la COVID-19 kuwa kikwazo kikubwa, na ambalo lilisababisha kiwango kikubwa cha watu kupoteza ajira.

Vilevile imegusia vita vya nchini Ukraine kuwa pia ni sababu ya kuongezeka kwa bei za chakula, nishati na mbolea, hali inayowatumbukiza mamilioni ya watu katika adha ya kukosa fursa za kujitafutia mlo wa kutosha.

Mashirika hayo ya Umoja wa mataifayamesema ni muhimu kufanyike marekebisho katika mifumo ya kilimo ili kuwezesha uzalishaji wa chakula chenye lishe bora na wakati huo huo kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa wote.