1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Faeser: Wafuasi wa Hamas wanapaswa kufurushwa Ujerumani

15 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema watu wanaoliunga mkono kundi la Hamas nchini Ujerumani wanapaswa kufurushwa kutoka nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4XYMk
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani - Nancy Faeser
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani - Nancy FaeserPicha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Faeser amesema watatumia njia zote za kisheria kuwafurusha wafuasi wa Hamas. Matamshi ya Faeser yameungwa mkono na kiongozi wa chama cha Social Democrat (SPD) Lars Klingbell ambaye ameliambia gazeti la shirika la habari la Funke kuwa ikiwa mtu anawaunga mkono Hamas hadharani na hana uraia wa Ujerumani, basi atafukuzwa kutoka nchini.

Kilingbell asema anayepinga maadili ya Ujerumani atanyimwa uraia

Klingbell ameongeza kuwa njia za kisheria zitatumikana na kwamba yeyote anayepinga maadili ya Ujerumani kama kuunga mkono ugaidi na chuki dhidi ya Wayahudi atanyimwa uraia wa Ujerumani.

Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani ikiwemo, pamoja na nchi nyingine kadhaa, zimeliweka kundi la Hamas kwenye orodha ya magaidi.