1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EVORA: Umoja wa Ulaya wahimizwa kuchangia majeshi

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLx

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Herve Morin amezihimiza nchi washirika wa umoja wa ulaya zichangie wanajeshi katika kikosi cha pamoja cha umoja wa mataifa na umoja wa ulaya cha kulinda amani nchini Chad na katika jamuhuri ya Afrika ya kati.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa ametoa mwito huo wakati ambapo mawaziri wa ulinzi wa umoja wa ulaya wanakutana mjini Evora- Ureno kwa mkutano wa siku mbili kujadili shughuli za kijeshi za umoja wa ulaya katika Bosnia pamoja na kutumwa wanajeshi wa kuwalinda wakimbizi wa Darfur, Chad na katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limepitisha azimio linaloruhusu kutumwa askari 300 wa umoja wa mataifa kusimamia kambi za wakimbizi wa Darfur na wengineo walio yatoroka makaazi yao.