1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yataka hukumu ya kifo ya Jamshid Shamrad ifutwe

29 Aprili 2023

Umoja wa Ulaya umesema "unalaani vikali", uamuzi wa mahakama ya Iran kutoa hukumu ya kifo kwa raia wa Ujerumani mwenye asili ya Iran

https://p.dw.com/p/4QhyX
Eu Flagge Flash-Galerie
Picha: AP Graphics

Jumatano iliyopita Mahaka ya Juu ya Iran ilithibitisha kutolewa kwa hukumu hiyo ya kunyongwa dhidi ya Sharmhad inayosubiri utekelezaji. Bado haijafahamika ni lini hasa hukumu hiyo itatekelezwa.

Soma zaidi:Ujerumani yakosoa hukumu ya kifo kwa raia wake, Iran

Katika taarifa yake ya jana Ijumaa Umoja wa Ulaya uliitaka Iran ifute hukumu hiyo na ihakikishe mtuhumiwa anapewa haki zake za msingi kwa kuzingatia sheria za kimataifa bila ya kuchelewa.

Itakumbukwa mwezi Februari mwaka huu mahakama ilimweka kizuizini mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 68 kwa tuhuma za kuhusika na shambulio la kigaidi, miongoni mwa mambo mengine. Lakini kimsingi amekuwa kizuizini tangu mwaka 2020.