1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yataka faini kubwa mahakamani katika kesi ya AstraZeneca

26 Mei 2021

Umoja wa Ulaya umeipeleka katika mahakama ya Brussels kampuni ya kutengeneza chanjo ya AstraZeneca na kuituhumu kutokuwa na nia njema katika kuyapa mataifa mengine dozi za chanjo hiyo.

https://p.dw.com/p/3u02f
AstraZeneca Covid-19 Impfung
Picha: Yui Mok/PA Wire/empics/picture alliance

Umoja wa Ulaya umeituhumu kampuni hiyo ya Uingereza na Marekani kwa kuchelewesha uuzaji wa chanjo hizo ili iihudumie Uingereza, miongoni mwa wengine.

Mkataba wa AstraZeneca iliosainiwa na Halmashauri Kuu ya Ulaya, kwa niaba ya mataifa wanachama ulihitaji kutolewa dozi za mwanzo milioni 300 kwa ajili ya kusambazwa miongoni mwa nchi 27, na chaguo la kuongeza dozi nyingine milioni 100.

soma zaidi: Je chanjo ya AstraZeneca ni salama?

Dozi hizo zilitarajiwa kutolewa katika mwaka mzima wa 2021. Lakini milioni 30 pekee zilitumwa wakati wa robo ya kwanza ya mwaka huu.

Utoaji wa dawa hizo umeongezeka kidogo tangu wakati huo, lakini Halmashauri Kuu ya Ulaya inasema AstraZeneca inatarajiwa kutoa dozi milioni 70 katika robo ya pili ya mwaka na ilhali ilikuwa imeahidi milioni 180.