1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kuiunga mkono Ukraine lakini kutoziba pengo la Marekani

6 Oktoba 2023

Umoja wa Ulaya umeapa kuiunga mkono Ukraine katika mkutano wa kilele Alhamisi lakini ukaonya kuwa Umoja huo hautaweza kuziba pengo lolote la ufadhili litakaloachwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4XBJq
Ursula von der Leyen / Rede 30.03.2023
Picha: VALERIA MONGELLI/AFP/Getty Images

Hofu hiyo imechochewa na mzozo wa kisiasa mjini Washington, uliopelekea Rais Joe Biden kukiri ya kuwa hali hiyo "inamtia wasiwasi" kwamba msaada wa Marekani kwa Ukraine huenda ukayumba. Umoja wa Ulaya na Marekani hutoa mabilioni ya fedha na msaada wa kijeshi kwa Kyiv.

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky amesema ana imani bado anaungwa mkono na pande zote nchini Marekani huku akisisitiza umuhimu wa misaada kutoka kwa mataifa ya Magharibi katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi.