1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU na Marekani zashindwa kutatua migogoro ya kibiashara

21 Oktoba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Umoja huo Charles Michel jijini Washington.

https://p.dw.com/p/4Xq7c
Washington Ursula von der Leyen bei US Präsident Biden
Picha: Al Drago/UPI/IMAGO

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Umoja huo Charles Michel katika mkutano wa kilele uliofanyika jijini Washington jana Ijumaa.

Viongozi hao walikutana kwa lengo la kujadili ushirikiano kwenye teknolojia mpya na muhimu, ikijumuisha miundombinu ya kidijitali na teknolojia ya akili bandia pamoja na masuala ya sera ya kibiashara. Hata hivyo viongozi hao walishindwa kutatua mizozo mikubwa ya kibiashara kati yake.

Duru zinasema pande zote mbili hazikuweza kukubaliana juu ya jinsi gani hasara za kiushindani kwa wasafirishaji wa ulaya wa chuma na alumini  kwenye soko la Marekani, zinaweza kuondolewa kwa muda mrefu.

Mazungumzo hayo muhimu pia yalitawaliwa na mzozo unaoendelea huko Gaza pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.