1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya yasema idadi ya waomba hifadhi yaongezeka

5 Septemba 2023

Idadi ya wahamiaji wanaoomba hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya imeongezeka kwa asilimia 28. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na shirika linalohusika na suala la uhamiaji la Umoja wa Ulaya EUAA.

https://p.dw.com/p/4VyKU
Großbritannien Proteste gegen die Abschiebung nach Ruanda
Picha: Niklas Hallen/AFP/Getty Images

Takwimu hizo zinaonesha idadi imeongezeka katika kipindi cha nusu ya mwanzo ya mwaka huu ambapo kati ya mwezi Januari na mwishoni mwa mwezi Juni  yalikuweko maombi 519,000 ya watu wanaotaka hifadhi katika nchi 27 za kanda hiyo na nchi nyingine washirika za Uswisi na Norway. 

Mpango wa Uingereza, Rwanda wa wahamiaji wakumbwa na kikwazo

Idadi ya walioomba hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya mwaka huu ndio kubwa zaidi kuwahi kuonekana tangu mwaka 2015-2016 wakati liliposhuhudiwa wimbi kubwa la wakimbizi wengi Wasyria waliokimbia vita nchini mwao.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa,Ujerumani imepokea asilimia 62 ya maombi yote ya hifadhi ya ukimbizi ya wasyria katika Umoja huo wa Ulaya ndani ya kipindi cha nusu ya mwaka huu.