1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yawazuwiya watigray waliofukuzwa Saudi Arabia

5 Januari 2022

Maafisa nchini Ethiopia wamewakamata kiholela na kusababisha kutoweka kwa maelfu ya watu wenye asili ya Tigray ambao hivi karibuni walifukuzwa kutoka Saudi Arabia

https://p.dw.com/p/45AGp
Saudi Arabien I Äthiopische Migranten werden in ihr Herkunftsland zurückgebracht
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti mpya ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch iliyotolewa huku mzozo mbaya wa Tigray ukiendelea.

Serikali ya Ethiopia imesema hatua hiyo inalenga watu wanaoshukiwa kuunga mkono vikosi vya Tigray ambao wanapambana na serikali tangu Novemba mwaka 2020. 

soma zaidi:Ethiopia yapitisha sheria ya kuanza tume ya majadiliano ya kitaifa

Ripoti hiyo iliyotolewa leo imetoa wito kwa maafisa wa Saudia "kuacha kuwashikilia watu wa kabila la Tigray katika mazingira ya kuchukiza na kuwarejesha nchini Ethiopia, na badala yake wawape ulinzi wa kimataifa.''

Maelfu ya Waethiopia, wengi wao kutoka mikoa ya Tigray na Amhara wamekuwa wakisafiri kimagendo kila mwaka hadi nchini Saudi Arabia kupitia Yemen katika dhamira ya kutafuta maisha bora. Lakini maafisa wa Saudi wamefurushwa maelfu yao katika miaka ya hivi karibuni.