1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yamuongezea mwaka mmoja Abiy

10 Juni 2020

Bunge la Ethiopia limeidhinisha kumuongezea mwaka mmoja waziri mkuu wa taifa hilo Abiy Ahmed baada ya uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwezi Agosti kuahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3dax8
Dr. Abiy Ahmed
Picha: DW/S. Teshome

Hatua hiyo imefikiwa siku mbili baada ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani kujiuzulu katika nafasi ya spika wa bunge kufuatia kupinga hatua hiyo.

Bunge lilipigia kura azimio ya kuwaongezea muda wabunge na shirikisho na majimbo pamoja na watendaji wakuu wa serikali kwa kati ya miezi tisa na 12 hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa bunge Gebru Gebreslassie alipozungumza na shirika la habari la Reuters. 

Uchaguzi utaendelea katika kipindi hicho mara baada ya mamlaka za afya kueleza kwamba janga la virusi vya corona sio tena kitisho cha kiafya kwa umma, amesema Gebru. Ethiopia ilirekodi visa jumla 2,336 vya COVID-19 na vifo 32 hadi Jumatano hii.(10.06.2020).

Norwegen l Verleihung des Friedensnobelpreis an Abiy Ahmed in Oslo
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli ya mwaka 2019, kutokana na juhudi zake za kurejesha demokrasia nchini EthiopiaPicha: picture alliance/AP Photo/NTB scanpix/H. M. Larsen

Keria Ibrahim aliyejiuzulu nafasi hiyo siku ya Jumatatu, ni afisa wa juu wa chama cha upinzani cha Tigray People's Liberation, TPLF kinachopinga maamuzi hayo yaliyofikiwa mwezi Machi ya kusogeza mbele uchaguzi kutokana na janga hilo.

Kuongezewa muda kwa Abiy kunaweza kuchochea kuongezeka kwa mzozo kati ya serikali na chama hicho cha TPLF, ambacho kimetishia kufanya uchaguzi wake katika jimbo la Tigray, ambako ni nyumbani mwa makundi ya kikabila yenye ushawishi mkubwa nchini Ethiopia.

Abiy aliingia madarakani mwanamo 2018 kuongoza taifa hilo la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika na tangu wakati huo amekuwa akifanya mageuzi mengi na kuruhusu uhuru mpana katika taifa hilo ambalo kwa muda mrefu lilikabiliwa na ukandamizaji mkubwa. Alishinda tuzo ya kimataifa ya amani ya Nobeli ya mwaka 2019.

Soma Zaidi: Abiy Ahmed wa Ethiopia akabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel

Mashirika: AFPE