1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki inasimama na Lebanon katikati ya mvutano na Israel

26 Juni 2024

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amesema nchi hiyo inasimama na Lebanon katikati ya mvutano wake na Israel na ameyahimiza mataifa ya ukanda huo kuiunga mkono Beirut.

https://p.dw.com/p/4hYEu
 Erdogan
Rais wa Uturuki Tayyip ErdoganPicha: Europa Press/ABACA/IMAGO

Katika hotuba aliyoitoa bungeni, Erdogan amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anapanga kuvitanua vita vya Gaza hadi eneo hilo.

Ameongeza kuwa mipango ya Netanyahu ya kuvitanua vita hivyo itasababisha kile alichokiita “janga kubwa” huku akikosoa uungwaji mkono wa mataifa ya magharibi kwa Israel.

Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua takriban 24 mjini Gaza

Mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah umeongezeka katika wiki za hivi karibuni, na kuzua hofu ya kutokea kwa vita kamili kati ya Israel na Hezbollah.