1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan aungwa mkono na mgombea mwenza

23 Mei 2023

Mgombea Urais aliyeshikilia nafasi ya tatu nchini Uturuki Sinan Ogan ametangaza jana jioni kumuunga mkono rais wa sasa Reccep Tayyip Erdogan.

https://p.dw.com/p/4RhPp
Türkei Wahlen Sinan Ogan und Recep Tayyip Erdogan
Picha: Turkish Presidency via AP/AP Photo/picture alliance

Hivyo kuongeza changamoto kwa mgombea wa upinzani Kemal Kilicdaroglu kabla ya duruya piliya uchaguzi siku ya Jumapili.

Licha ya kutokuwa maarufu kabla ya kampeni, Ogan anayeegemea upande wa siasa kali za kizalendo alipata asilimia 5.2 ya kura katika uchaguzi wa Mei 14.

Soma pia; Erdogan aahidi kukabidhi madaraka iwapo atashindwa uchaguzi

Amesema kuwa muungano wa Kilicdaroglu ulishindwa kumshawishi kuhusu mustakabali wa taifa hilo na kusisitiza kuwa uamuzi wa kumuunga mkono Erdogan umetokana na mapambano yake yasiyokoma dhidi ya ugaidi.

Erdogan ambaye analenga kuendeleza utawala wake kwa muongo mmoja zaidi, alipata asilimia 49.5 na chama chake kupata wingi wa viti Bungeni. Mpinzani wake mkuu alijizolea asilimia 44.9 ya kura.