1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan ashauri kuunda tume kuchunguza mkasa wa bwawa

7 Juni 2023

Rais Erdogan wa Uturuki leo ametoa pendekezo la kuundwa jopo la kimataifa kuchunguza kisa cha kushambuliwa kwa kombora, bwawa kubwa la maji nchini Ukraine, mkasa uliosababisha maafa ya kutisha kusini mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4SJQH
Türkei I Erdogan I Bekanntgabe Kabinett
Picha: Umit Bektas/REUTERS

Kiongozi huyo ametoa pendekezo hilo alipozungumza kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti na Rais Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Kwa mujibu wa ikulu ya Uturuki, Erdogan, ametanabahisha viongozi hao wawili kuwa uchunguzi huru na kina unahitajika ili kubaini ukweli wa kushambuliwa kwa bwawa la Kakhovka.

Erdogan ameshauri kwamba jopo la wachunguzi linaweza kuwajumuisha maafisa wa Umoja wa Mataifa na Uturuki.

Tangu kutokea mkasa huo hapo jana, Ukraine na Urusi zimeshutumiana kwa kila upande kuulaumu mwingine kuhusika na uharibifu wa bwawa hilo uliosababisha mafuriko yasiyo mfano kusini mwa Ukraine.