1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan anatarajiwa kuapishwa tena kama rais wa Uturuki

3 Juni 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anaapishwa mjini Ankara kuendelea kushikilia wadhifa wake baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4S9dA
Türkischer Präsident Rcep Tayyip Erdogan | Ankara, Türkei
Picha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Erdogan, anayeingia kwenye muhula wa tatu madarakani, anatarajiwa kulitangaza baraza lake la mawaziri baada ya sherehe za uapisho. Katika uchaguzi wa wiki iliyopita uliomuweka madarakani, Rais huyo wa Uturuki aliungwa mkono kwa asilimia 52. 

Sherehe za uapisho zitafuatiwa na hafla itakayofanyika katika kasri la Rais na inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa 78, na mashirika ya kimataifa. 

Erdogan ashinda duru ya pili ya uchaguzi Uturuki

Kulingana na shirika la habari la Uturuki, Anadolu, katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, rais wa Venezuela Nicolas Maduro, waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban na wa Armenia Nikol Pashinyan, ni miongoni mwa watakaoshiriki kwenye hafla hiyo