1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan ataka mahusiano ya Uturuki-China yaimarike

4 Julai 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, leo amemwambia mwenzake wa China Xi Jinping kwamba anataka hatua za kuboresha uhusiano kati ya Uturuki na China katika nyanja zote kuendelea.

https://p.dw.com/p/4hsEU
Rais Erdogan wa Uturuki
Rais Erdogan anataka kuimarisha mahusiano kati ya Uturuki na ChinaPicha: Europa Press/ABACA/IMAGO

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, leo amemwambia mwenzake wa China Xi Jinping kwamba anataka hatua za kuboresha uhusiano kati ya Uturuki na Chinakatika nyanja zote kuendelea, na kuongeza kuwa anaamini hatua hiyo itakuwa na manufaa kwa nchi zote mbili. Haya ni kulingana na ofisi ya Rais wa Uturuki.

Katika taarifa, ofisi hiyo imesema kuwa viongozi hao wawili, walikutana wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) unaofanyika kwenye mji mkuu wa Kazakhstan, Astana, na kuzungumza kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine pamoja na mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Erdogan ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti na jumuiya ya kimataifa kuzuia kuenea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati.