1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England yaingia nusu fainali ya ligi ya mataifa

Sekione Kitojo
19 Novemba 2018

Uhispania yanyang'anywa nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la ligi ya mataifa ya Ulaya na kikosi cha England.

https://p.dw.com/p/38Xbz
Fußball WM 2018 Kolumbien vs England
Gareth SouthgatePicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Nchini  Uingereza  kocha  Gareth Southgate amekitaka  kikosi  chake cha  vijana  chipukizi  kuendelea  na  kasi  hiyo  hiyo  ya  mwaka  huu wakati  wakinyakua  nafasi  katika  michuano  ya  nusu  fainali  ya Ligi  ya  mataifa. Croatia  wakati  huo  huo, imeshuka  kutoka  ligi A miezi minne baada  ya  kufika  fainali  ya  kombe  la  dunia  kule Urusi.

UEFA Nations League | England vs. Kroatien
Wachezaji wa England wakipongezana baada ya kupata baoPicha: Reuters/D. Klein

Kufuzu  kucheza  mashindano ya  timu  nne  mwezi  Juni mwakani  ni  hatua  nyingine  ya  maendeleo  makubwa  kikosi  cha England yalichofanya  chini  ya  kocha  Southgate ambayo  yalianza kwa  kufikia  nusu  fainali  ya  kombe  la  dunia  katikati  ya  mwaka huu.

Ushindi  wa  Croatia  dhidi  ya  Uhispania  wiki  iliyopita uliweka pambano  ya  Jumapili  kuwa  muhimu  kwa  kila  timu, ambapo timu yeyote  ilikuwa  na  uwezo  wa  kushinda  kundi  hilo  ama  kushuka daraja. 

England  ilifanikiwa  kushinda  pambano  hilo  la  Jumapili kwa  ushindi  wa  mabao 2-1  dhidi  ya  Croatia  na  kuiwezesha England  kusonga  mbele.

Schriftzug UEFA Nations League auf Werbebande
Picha: picture-alliance/augenklick/firo Sportphoto

Ubelgiji  hawakuweza  kuelezea  hali  yao  ya  kuporomoka  dhidi  ya Uswisi  jana  Jumapili, wakati  walipopoteza  nafasi  ya  uongozi  wa mabao 2-0, na  kubugia  mabao matano  na  kukosa  nafasi  ya kuingia  katika  timu  nne  bora  za  ligi  ya  mataifa ya  Ulaya.

Baadhi  ya  wachezaji  walihisi kikosi  hicho  kilichofikia  nusu  fainali ya  kombe  la  dunia  kilijibweteka  baada  ya  kuongoza  kwa mabao 2  katika  muda  wa  dakika 17  za  mchezo.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / ape / afpe / rtre

Mhariri:  Yusuf , Saumu