1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

El Baradei ataka kuandaa ukaguzi silaha huko Libya:

27 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFol
VIENNA: Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea, Muhammed El Baradei, hii leo atakwenda katika mji mkuu wa Libya, Tripolis kwa madhumuni ya kuandaa ukaguzi wa silaha wa mabingwa wa Shirika lake nchini Libya. Taarifa za shirika lake hilo zilisema kuwa safari ya El Baradei itachangia katika ukaguzi wa harakati zote za kinyuklea za nchi hiyo. Rais Muammar al Ghaddafi wa Libya hapo Disemba 19 alifikia mapatano pamoja na Marekani na Uingereza juu ya kuteketezwa silaha zote za kuangamiza za nchi yake.