1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW yazungumza na Rais Samia wa Tanzania

17 Februari 2022

Idhaa ya Kiswahili ya DW imefanya mahojiano maalum na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa yuko mjini Brussels, Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa kilele kati ya viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/479Uk

Katika mahojiano hayo aliyofanyiwa na Sudi Mnette, Rais Samia amezungumzia masuala kadhaa ikiwemo matarajio yake kuhusu mkutano huo, uhusiano kati ya Tanzania na Ulaya, kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe na mazungumzo yake na makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anayeishi uhamishoni nchini Ubelgiji.

Kwa mahojiano zaidi tembelea chaneli yetu ya Youtube ambako utaona pia vidio kuhusu mahojiano hayo.