1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI:Kiongozi wa Al-Qaeda,Saudi Arabia auawa.

18 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjt

Mtu mmoja anayedhaniwa ni kiongozi wa mtandao wa kikundi cha kigaidi cha Al-Qaeda nchini Saudi Arabia,Saleh al Ufi,ameuawa leo baada ya kutokea mapigano kati ya polisi na wapiganaji wa kikundi hicho katika mji mtakatifu wa Medina.

Saleh al-Ufi,ambaye alikuwa akisakwa kwa udi na uvumba,akiwa ni mmoja kati ya watu wawili walio katika orodha ya watu 26 ambao bado wanasakwa.Mtuhumiwa mwengine Taleb Al-Taleb bado yupo mafichoni.

Mkuu mpya wa kikundi cha Al-Qaeda nchini Saudi Arabia raia wa Morroco,Younes Mohammed Ibrahim Al-Hayari,aliuawa katika mapigano na polisi katika mji mkuu wa Saudi Arabia,Riyadh tarehe 3 mwezi uliopita wa Julai.

Taarifa iliyotolewa na televisheni ya Saudia,imeeleza kuwa mapema vikosi vya usalama viliwakamata watuhumiwa kadhaa wa ugaidi katika mji wa Medina.Kabla ya hapo vikosi hivyo vya usalama viliwauwa wanamgambo wanne,katika mapigano yaliyotokea alfajiri mjini Riyadh.