1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI. Viongozi wa kundi la Jamaa Islamiya la Misri wajiunga na Al Qaeda

6 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDOR

Kaimu kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahiri amesema kwamba wawakilishi kadhaa wa kundi la wapiganaji la Jamaa Islamiya kutoka nchini Misri wamejiunga na mtandao wa kimataifa wa kundi la Al qaeda.

Televisheni ya Al Jazeera imeonyesha ukanda wa video ambapo Al Zawahiri aliwapongeza wafuasi hao wapya.

Jamaa Islamiya ndio kundi kubwa zaidi la wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali nchini Misri.

Kundi hilo lilihusika na mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa Misri Anwar Sadat mwka 1981.