1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI: Makamu wa Bin Laden ametoa ujumbe mpya

30 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7S

Naibu kiongozi wa mtandao wa kigaidi,Al-Qaeda,Ayman al-Zawahiri amejitokeza upya na ujumbe kwenye ukanda wa video uliotolewa katika mtandao wa Internet.Makamu wa Osama Bin Laden amemlaani Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 kwa matamshi yake ya hivi karibuni kuhusu Uislamu. Zawahiri katika ujumbe wake akaendelea kusema kuwa rais George W.Bush wa Marekani ni mwongo kwani anaona maendeleo katika vita dhidi ya ugaidi.Ukweli wa mambo ni kwamba katika miaka mitatu na nusu iliyopita,mtandao wa Al-Qaeda ndio uliozidi kuwa na nguvu,aliongezea makamu wa Bin Laden.