1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI: Kundi la Al-Qaeda latishia kufanya mashambulio

27 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3W

Huku hasira miongoni mwa mataifa ya kiarabu ikizidi juu ya hatua ya Israel kuishambulia Lebanon na eneo la Ukanda wa Gaza, kundi la al-Qaeda limetangaza halitakaa kimya. Hata hivyo kundi hilo halikutaja ni kitu linachopania kukifanya.

Naibu kiongozi wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahri, amesema kwenye runinga ya Al Jazeera kwamba kundi lake haliwezi kuangalia huku mabomu yakiwanyeshea walebanon na wapalestina kama mvua.

Mwanamgambo huyo mzaliwa wa Misri amewataka waislamu ulimwenguni kote kupigana na kuwa mashahidi katika vita dhidi ya Wayahudi na Wamarekani.

Haya ni matamshi ya kwanza ya kundi la al-Qaeda lililo na idadi kubwa ya Wasunni dhidi ya Israel inayolishambulia kundi la wanamgamo wa kishia la Hezbollah.