1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

DRC yasusia mkutano wake na Rwanda huko Qatar

23 Januari 2023

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imesusia mkutano ulioitishwa na Qatar kwa lengo la kuutafutia ufumbuzi mvutano uliopo kati ya nchi hiyo na jirani yake Rwanda.

https://p.dw.com/p/4Mb8i

Duru zinasema mkutano huo uliopangwa kufanyika siku ya Jumatatu mjini Doha, chini ya upatanishi wa taifa hilo la Ghuba umefutwa dakika za mwisho baada ya Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi kutofanya safari kwenda nchini Qatar. Sababu gani hasa huenda zimechochea msimamo huo wa serikali ya Kongo? Swali hilo na mengine Rashid Chilumba amemuuliza Ali Mali, mchambuzi wa siasa za Maziwa Makuu.