1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yasema haitaruhusu madini yake kuchakatwa nje ya Afrika

4 Novemba 2021

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema haitaruhusu tena madini ya nchi hiyo kuchakatwa nje ya Afrika kwani inataka utajiri wake wa madini kuwasaidia Wakongomani pamoja na Waafrika.

https://p.dw.com/p/42ash
Kirgisistan Kumtor Mine
Picha: Tabyldy Kadyrbekov/dpa/picture alliance

Waziri wa Viwanda Julien Paluku Kahongya, amewaambia waandishi wa habari kwamba Kongo itawakutanisha hivi karibuni, viongozi wa nchi kadhaa za Afrika zinazomiliki midogi ya madini ndani ya ardhi yao, ili kuchunguza vipi wao wenyewe wataanza kuyachakata madini hayo barani Afrika.

Kongamano hilo lililopewa jina la "DRC-Africa Business" linatarajiwa kufanyika mjini Kinshasa tarehe 24 hadi 25 mwezi huu na litahudhuriwa na wawakilishi 1,000 wa sekta za magari, benki na biashara.

Utafiti kuhusu madini yaliyomo ndani ya ardhi ya Kongo na matumizi yake tayari umeshafanywa na wataalamu wa kampuni Bloomberg.

Waziri Paluku amesema miaka kumi ijayo, magari milioni 145 yatatengenezwa kupitia madini ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.