1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ipi maana ya siku ya ukombozi DRC?

17 Mei 2022

Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo inaadhimisha miaka 25 tangu vita vilivyoongozwa na hayati Laurent Désiré Kabila kumuondoa madarakani Mobutu Seseseko. Lakini wakongo bado wanajiuliza maana ya siku hii ya "ukombozi".

https://p.dw.com/p/4BQZF
Präsident Mobutu
Picha: dpa/picture alliance

Wanajeshi wa AFDL walipoingia katika mji mkuu Kinshasa mnamo mei 17 mwaka elfu moja mia tisa tisini na saba (1997). Laurent-Désiré Kabila, ambaye alikuwa msemaji wake, alijitangaza kuwa rais mpya wakati huo kutoka Lubumbashi, kumfukuza Mobutu Seseseko aliyetawala kwa muda wa miaka thelasini na mbili.

Askari wa AFDL ambao baadhi yao walikuwa watoto wenye umri wa miaka chini ya kumi na mnane walioitwa "Kadogo” waliingia kwa ushindi katika mji mkuu Kinsasa nchini Zaire, nchi ambayo baadae ilibadilishwa jina kuwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Hérita Mbulanga ni miongoni mwa askari wa "Kadogo” wa wakati ule, kwasasa akiwa mwanachama cha upinzani cha AFBC kinamuunga mkono rais wazamani Joseph Kabila anasema alikuwa na miaka 14 wakati alipofunzwa namna ya kutumia silaha.

Upande wa chama tawala, wanachama wana.zinyooshea pia kidole kasoro nyingi zilizo tokea baada ya ukombozi ule uliomfurusha rais Mobutu, wakidai kwamba kwasasa rais Félix Tshisekedi anafanya juhudi zote kurekebisha.

Hata hivyo, mwanaharakati wa haki za kibinadamu Jean-Moreau Tubibu anahisi kwamba ukombozi wa Congo umefanyika, akiwataja raia wa Congo kuwajibika kwa kuilinda  nchi yao.

Siku hii imetangazwa kuwa siku ya ushindi wa jeshi nchini Congo, na ni siku ya mapumziko.Gwaride mbalimbali zimefanyika katika mikoa kadhaa ya Congo huku askari wakihimizwa kulinda nchi yao inavyo stahili.

Mwandishi: Mitima Delachance, DW Bukavu