1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo, Rwanda zashutumiana majibizano ya risasi mpakani

16 Februari 2023

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda zimeshtumiana kuhusu tukio la ufyatuaji risasi mpakani.

https://p.dw.com/p/4NY3U
Ruandas Präsident Paul Kagame Felix und DR Kongos Präsident Tshisekedi
Picha: Simon Wohlfahrt/AFP

Rwanda limesema wanajeshi kati ya 12 na 14 wa Kongo waliingia katika eneo linalozitenganisha nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa mwanajeshi wa Kongo alifyatua risasi kwenye kituo chao cha mpakani.

Katika kujibu tuhuma hizo, gavana wa mkoa wa Kongo wa Kivu Kusini, Theo Ngwabidje, alizitaja kuwa ni uongo, lakinialithibitisha kwamba tukio limetokea mpakani.

Soma pia:Mlinda amani wa UN auawa Kongo

Hata hivyo alilielezea tukio hilo kama ugonvi uliohusisha ufyatulianaji wa risasi kati ya vikosi vya Kongo na wahalifu waliokuwa wanakimbia.

Tukio hilo limejiri katikati mwa mzozo kuhusiana na mashambulizi ya kundi la M23 kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini.

Serikali mjini Kinshasa inaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji hao, madai ambayo yanaungwa mkono pia na wataalam wa Umoja wa Mataifa na mataifa kadhaa ya magharibi, lakini yakipingwa vikali na Kigali.