1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yamsajili Sule kutoka Bayern

9 Februari 2022

Borussia Dortmund itamsajili beki wa kati wa Bayern Munich Niklas Sule bila ada yoyote mwishoni mwa msimu huu. Dortmund ilisema imekubaliana na Sule mwenye umri wa miaka 26 mkataba wa miaka minne.

https://p.dw.com/p/46kiR
Deutschland 1. Bundesliga Der Spieler Niclas Suele
Picha: Oryk HAIST//Sven Simon/imago images

Hii ni baada ya Sule kuamua kutorefusha kandarasi yake na mahasimu wakubwa wa Dortmund, Bayern Munich.

Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc amefurahishwa na usajili huu, "tunafurahia kwamba tumeweza kumsajili Niklas Sule kwa mkataba wa miaka minne," alisema Zorc.

Bayern kwa upande wao wiki iliyopita walisema Sule ataihama klabu hiyo baada ya kukataa mkataba mpya waliompendekezea.

Tangazo hili ni habari njema kwa mashabiki wa Dortmund hasa baada ya kushinidiliwa magoli matano na Bayer Leverkusen katika uwanja wao wa nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita.