1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund na mtihani mkubwa katika Champions League

4 Machi 2019

Borussia Dortmund wanashuka dimbani uwanjani Signal Iduna Park kupambana na Tottenham Hotspur katika mechi ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 za mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

https://p.dw.com/p/3EPnF
UEFA Champions League Achtelfinale | Tottenham Hotspur vs. Borussia Dortmund | 3. TOR Tottenham
Picha: Reuters/M. Childs

Borussia Dortmund wanashuka dimbani uwanjani Signal Iduna Park kupambana na Tottenham Hotspur katika mechi ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 za mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Na wakati BVB walizabwa mwishinoni mwa wiki 2 - 1 na Augsburg, wapinzani wao Tottenham Hotspur walikuwa na mechi kali ya watani wa Kaskazini mwa London ambapo walitoka sare ya 1 – 1 na Arsenal.

Kwingineko, vichapo viwili mfululizo mikononi mwa Barcelona vimeiacha Real Madrid na fursa moja tu ya kuuokoa msimu wao kwa kuweka rekodi ya kushinda Kombe la nne mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini lazima wafanye hivyo bila ya mabao ya Cristiano Ronaldo, mshambuliaji nyota ambaye aliwasaidia sana katika ubingwa huo kabla ya kuhamia Juventus mwishoni mwa msimu uliopita.

Madrid ilishindwa kufunga bao dhidi ya Barcelona katika mechi mbili za Classico dimbani Santiago Bernabeu katika wiki moja.

Na sasa watahitaji kurejesha fomu yao nzuri watakapowaalika Ajax wa Uholanzi. Walishinda mechi ya ugenini 2 – 1 yaliyofungwa na Karim Benzema na Marco Asensio.

Timu nyingine itakayokuwa na mlima wa kukwea ni Manchester United ambayo inasafiri kwenda Paris Jumatano kujaribu kugeuza kichapo cha 2 – 0 mikononi mwa Paris Saint Germain.

Katika mechi nyingine ya Jumatano, FC Porto watakuwa wenyeji wa AS Roma ambao walishinda mechi ya kwanza 2 – 1