1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Diwani wa zamani wa Rukara nchini Rwanda anasemekana hana hatia

13 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCi

Korti kuu ya kimataifa inayowahukumu waasisi wa mauwaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda, imefuta mashtaka dhidi ya diwani wa zamani Jean Mpambara.Ushahidi uliokusanywa umedhihirisha diwani huyo aliwasaidia zaidi wahanga.Hukumu ya korti kuu ya kimataifa ya Arusha inasema diwani huyo ,badala ya kuihama Rwanda pamoja na wakimbizi wengineo,aliamua kusalia na kuwapatia vitambulisho watutsi vinavyoonyesha kua wao ni wahutu, ili waweze kukiuka vizuwizi bila ya kusumbuliwa.Jean Mpambara alikua diwani wa Rukara.Wakati huo huo mkuu wa zamani wa kijeshi kanali Tharcisse Muvunyi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa kuhusika na mauwaji ya halaiki na kuchochea mauwaji ya Butare ambako zaidi ya watu laki moja waliuwawa.