1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuinea

Dikteta wa Guinea ahukumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu

1 Agosti 2024

Kiongozi wa kijeshi wa zamani nchini Guinea ya Conakry Moussa Camara amehukumuwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya mahakama ya mjini Conackry kumpata na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

https://p.dw.com/p/4izr1
Moussa Camara katika mwaka wa 2009
Moussa Camara aliitawala Guinea kutoka 2008 hadi 2010Picha: SCHALK VAN ZUYDAM/AP/picture alliance

Kiongozi wa kijeshi wa zamani nchini Guinea ya Conakry Moussa Camara amehukumuwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya mahakama ya mjini Conackry kumpata na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Soma pia: Kiongozi wa zamani wa Kijeshi wa Guinea atoroshwa gerezani

Camara alihukumiwa Jumatano kwa mauaji ya watu 157 mnamo mwaka 2009.  Wanajeshi waliwaua watu hao katika uwanja wa michezo mjini Conackry ambapo wanawake kadhaa pia walibakwa.   

Mahakama ya Jinai nchini humo ilimtia hatiani Camara na maafisa wengine saba wa ngazi ya juu baada ya kusikilizwa kesi hiyo ya mauaji, utekaji nyara na ubakaji iliyochukua muda mrefu. Washtakiwa wanne waliachiliwa huru.

Soma pia:Viongozi wa kiraia waachiwa huru Guinea 

Zaidi ya watu 100 walionusurika na jamaa za waathiriwa walitoa ushahidi katika kesi hiyo iliyoanza Novemba mwaka 2022.