1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhamana wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa akiri aliwahi kupokea hongo

9 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmc

Dhamana wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa amekiri aliwahi kuhongwa.Mdhamini wa zamani wa shughuli za ununuzi za Umoja wa mataifa,Alexander JAKOWLEW wa Rashia amekiri aliwahi kupokea hongo ya karibu dala milioni moja katika mikakati ya kugawa mikataba ya kazi.Anasemekana amekiri pia kuhusika na visa vya udanganyifu na kubadilisha fedha kinyume na sheria.Umoja wa mataifa,umeamua kumpokonya kinga ya ubalozi mwanadiplomasia huyo wa Rashia.Akikutikana na hatia Alexander Jakowlew atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela.