1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhaka: Maandamano ya umma wa watu nchini Bangladesh wakitaka uchaguzi uahirishwe.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHi

Bangladesh inakabiliwa na michafuko zaidi huku maelfu ya watu wanajitayarisha kuandamana hadi katika Kasri la Rais katika jitihada ya kuilazimisha serekali iifute uchaguzi uliopangwa kufanywa mwezi huu. Huku mgomo wa usafiri nchini kote ukiingia siku yake ya tatu, wanachama wa chama kikuu cha upinzani na washirika wao wanatazamiwa kuandamana hadi Kasri la Rais, licha ya kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku kufanyika katika eneo hilo. Polisi na wanajeshi walikuwa wanapiga doria katika mji mkuu wa Dhaka wakijaribu kuyakomesha maandamano ya michafuko yaliodumu siku mbili sasa. Polisi wa kuzuwia fujo wametumia risasi za raba na hewa ya kutoa machozi katika mikasa hiyo.