1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya shambulizi la Hamas vyafikia watu 500

8 Oktoba 2023

Idadi ya waliouwawa kutokana na mashambulizi makubwa ya kushtukiza ya wapiganaji wa Hamas dhidi ya Israel imefikia watu 500.

https://p.dw.com/p/4XGaA
Israel Nahostkonftlikt l israelischer Soldat patrouilliert bei der Polizeistation in Sderot
Picha: Ronen Zvulun/REUTERS

Taarifa hiyo ni kwa mujibu ya  vyanzo vya kitabibu.Na Wizara ya Afya ya Israel imesema waliojeruhiwa ni 2,048 huku wengi miongoni mwa hao wakiwa katika hali mbaya. Kufuatia shambulizi hilo, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema baraza la usalama la Israel limetangaza hali ya vita kwa lengo la kutoa nafasi ya kuchukuliwa kwa hatua mbali mbali za kijeshi.Kundi la Hamas, ambalo linatawala Ukanda wa Gaza, lilifanya mashambulizi ya kushtukiza kutoka eneo la pwani jana Jumamosi ambayo yalihusisha kuvurumisha maroketi zaidi ya 3,000 katika ardhi ya Israel.Wapiganaji wa Hamas pia walivuka mpaka kwa kupitia nchi kavu, angani na baharini. Kwa mujibu wa jeshi la Israel, raia kadhaa wa Israel wamechukuliwa mateka na wanashikiliwa katika eneo la Gaza na wanamgambo wa Hamas.