1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dawa zakaribia kumalizika Sudan

4 Oktoba 2021

Serikali ya Sudan imesema inakaribia kuishiwa dawa muhimu, mafuta na ngano baada ya maandamano ya kisiasa kulazimisha kufungwa kwa bandari ya Sudan, ambayo ndiyo bandari kuu ya mashariki mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/41FBf
Sudan Karthoum | Anti-Regierungsproteste
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Wanachama wa kabila la Beja mashariki mwa Sudan wamezuwia barabara na kulazimisha bandari za Bahari ya Sham kufunga katika wiki za karibuni, kupinga kile wanachosema ukosefu wa mamlaka ya kisiasa katika eneo hilo, pamoja na hali duni ya kiuchumi.

Baraza la mawaziri lilikiri kuhusu madai ya haki ya eneo hilo, na kusisitiza haki ya kuandamana kwa amani:

Hata hivyo, lilionya kuwa kufungwa kwa bandari ya Sudan na barabara kuu zinazounganisha upande wa mashariki na maeneo mengine ya nchi kulikuwa kunaumiza maslahi ya Wasudan wote.