1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM:Rais wa Zanzibar atetea marufuku ya kufanyika mikutano ya kisiasa kwenye viwanja vya michezo

17 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaB

Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ametetea hatua ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya hadhara katika baadhi ya viwanja visiwani humo.

Uamuzi wa kukataza kufanyika mikutano ya hadhara ya kisiasa katika viwanja vya michezo uliotolewa na mkuu wa mkoa mapema ulishutumiwa na vyama vya upinzani na kutajwa kuwa jaribio la kutatiza kampeni.

Rais Karume alisema kuwa anaunga mkono hatua hiyo kwa kuwa mikutano hiyo inaingilia shughuli za viwanja hivyo.

Chama kikuu cha Upinzani Zanzibar CUF kimesema kitapuuza uamuzi huo na kitaendelea kufanya mikutano ya kampeni kwenye viwanja hivyo.

Nusura wafuasi wa CUF wakabiliane na wenzao wa chama tawala CCM walipowakuta wakicheza mpira katika uwanja walichotarajia kufanya mkutano wao wa kisiasa.