1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Watalii hawajulikani waliko kisiwani Zanzibar

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtK

Watalii wanne raia wa Danemark na mwalimu wao raia wa Canada hawajulikani waliko baada ya kufanya mafunzo ya kupiga mbizi mashariki mwa visiwa vya Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni la Swahali Divers, watu hao waliondoka pamoja na kundi lengine Jumamosi mchana na walionekana mara ya mwisho wakiwa majini karibu na kisiwa cha Pemba.

Baadhi ya vifaa vyao vilipatikana kazkazini mwa Pemba. Maofisa wa usalama na wananchi wanashirikiana kuwatafuta wahanga hao kutumia madau na ndege za makampuni ya kibinafsi.