1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Wakimbizi waanza kurejea makwao.

13 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbn

Karibu wakimbizi 14,000 wa Burundi wamerejea nyumbani mwezi uliopita kutoka katika makambi katika nchi jirani ya Tanzania , ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya idadi ya watu waliorejea mwezi July.

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa kiasi cha wakimbizi 13,746 walirejea kwa hiari yao nchini mwao mwezi wa August, ikiwa ni ongezeko la wakimbizi 5,399 waliorejea mwezi wa July.

Baada ya uchaguzi wakimbizi wengi wanataka kurejea nyumbani na shirika hilo linawasaidia , amesema afisa mmoja , na kuongeza kuwa shirika hilo hadi sasa limefanikisha kurejea kwa wakimbizi wapatao 185,333, tangu kuanza kwa zoezi hilo mwezi March 2002.