1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Viwanja vya michezo marufuku kufanyiwa mikutano.

19 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZd

Rais wa Zanzibar ametetea hatua ya kulazimisha mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kufanyika katika sehemu moja mjini Zanzibar, akisema kuwa hatua hiyo ina nia ya kulinda michezo kwa vijana.

Uamuzi uliotolewa na mkuu wa mkoa wiki hii kupiga marufuku matumizi ya viwanja vya michezo katika mikutano ya vyama vya siasa umelalamikiwa sana na vyama vya upinzani kuwa ni hatua ya kuzuwia vyama hivyo kufanya kampeni.

Wakati huo huo polisi wa Tanzania wamewafungulia mashtaka watu watano kwa madai ya kuuwa baada ya afisa mwandamizi wa chama tawala nchini humo kuuwawa katika tukio la kuchomwa moto.

Msemaji wa polisi amesema kuwa watu hao waliofanya kitendo hicho walimfungia ndani ya nyumba yake na kuchoma moto nyumba hiyo Mwajuma Nyanza , katibu mwenezi wa tawi la chama tawala CCM, mjini Dar Es Salaam mapema mwezi huu. Maafisa wa CCM wamesema kuwa shambulio hilo linaweza kuhusishwa na masuala ya kisiasa wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mkuu hapo Oktoba 30.