1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Upinzani wataka wabunge wasishirikiane na serikali.

6 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELM

Chama cha upinzani cha Zanzibar nchini Tanzania kimewataka wabunge wake waliochaguliwa kutoshirikiana na serikali baada ya kile inachosema kuwa ni udanganyifu katika uchaguzi uliokirejesha tena chama tawala nchini humo madarakani katika kisiwa hicho cha kitalii.

Chama cha upinzani cha Civic United Front CUF, kinaonekana kuacha nia yake ya hapo kabla ya kufanya maandamano makubwa dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili iliyopita ambao umegubikwa na siku kadha za mapambano kati ya wafuasi wa chama hicho cha CUF na polisi. Mtu mmoja anasemekana amekufa kutokana na ghasia hizo na wengine kadha wamejeruhiwa.