1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Uchaguzi kufanyika Oktoba.

9 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYT

Tanzania ambayo ilikumbwa na machafuko ya kisiasa baada ya uchaguzi wake mkuu mwaka 2000, itafanya tena uchaguzi wa rais na wabunge ifikapo Oktoba 30 mwaka huu.

Maafisa wa serikali ya Tanzania wamesema leo kuwa rais wa sasa Benjamin William Mkapa hatagombea baada ya kushika wadhifa huo kwa vipindi viwili, ikiwa ni uchaguzi wa tatu wa vyama vingi tangu pale nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka Uingereza wakati huo ikiitwa Tanganyika mwaka 1961.

Chama chake cha mapinduzi CCM, ambacho kimeiongoza nchi hiyo ya Afrika mashariki kwa zaidi ya miongo minne kinatarajiwa na wengi kushinda uchaguzi huo.