1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Semanza apewa kifungo cha miaka 35 badala ya 25

22 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBR

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayowashtaki wapangaji wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda,imeongeza hukumu ya meya wa zamani kwa miaka 10 zaidi,ikitupilia mbali rufaa yake na kugunduwa kwamba alikuwa pia anawajibika zaidi kwa mauaji yaliotokea kwenye mji wake.Hukumu hiyo ya kitengo cha rufaa cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Rwanda humaanisha kwamba Laurent Semanza,meya wa zamani mwenye umri wa miaka 61 sasa atumikie kifungo cha miaka 35 gerezani badala ya 25.