1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM : Rais wa Burundi akutana na kiongozi wa waasi wa FNL

15 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDI

Rais wa Burundi amekuwa na mazungumzo yake ya kwanza leo hii na kiongozi wa kundi pekee la waasi linaloendeleza mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muongo mmoja nchini humo.

Mkutano kati ya Rais Domitien Ndayizeye na kiongozi wa kundi la Kihutu la FNL Agathon Rwasa una lengo la kuwaingiza waasi hao kwenye mchakato wa amani.

Viongozi hao wawili wamekutana katika makao ya Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam kabla ya kuelekea hoteli kwa mazungumzo kufuatia mazungumzo ya faragha ya miezi kadhaa kati ya Tanzania na waasi hao wa FNL.